Jopo maalum la makocha ambao huchagua
wachezaji bora kwa kila mchezo kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara
wametoa matokeo ya wachezaji waliochaguliwa kuwa bora kwenye ligi hiyo
kwa mwezi April.
Mshambuliaji wa Yanga na timu ya Taifa, Mrisho Ngassa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom ya mwezi April.
Ngassa ametajwa kuwa mshindi katika nafasi hiyo, wenzake ambao walikuwa wakishiriki ni pamoja na mchezaji Amos Edward, Frank Domayo na Emmanuel Okwi baada ya kupata alama nyingi za mchezaji bora kwa kila mchezo.
Mbali na Ngassa pia James Ambrose ametajwa kuwa mchezaji bora wa Ligi hiyo kwa mwezi March 2015.
Zawadi ambayo watapatiwa mastaa hao kila
mmoja ni pesa kiasi cha Tshs. Mil. 1 kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo
kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.
0 comments:
Post a Comment