Kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM kulikuwa na msanii Banana Zorro akiwa na bendi yake ya B Band..
Unajua wasanii nao huwa wanaishi maisha ya kawaida kama watu wengine tu
mtaani, kuna wakati wanakutana na Hekaheka pia yani !!
Kabla ya kusimulia Hekaheka yake, Banana amepiga
story kuhusu ishu ya wasanii wa zamani kupotea, mwenyewe amesema
wanamuziki wa sasa wana umaarufu lakini hawajafikia uwezo wa wanamuziki
wa zamani.
Tukija kwenye Hekaheha aliyokutana nayo Banana amesimulia ishu aliyowahi kukutana nayo zamani wakati anaishi kwenye mtaa mmoja unaoitwa Kambauone na rafiki yake.. kilichomkuta ni kwamba huo mtaa ukileta mbwembe wanakufanyia mambo ya kiswahili.
Banana amesema aliwahi kushuhudia gari likinasa kibarazani, ikampa hofu sana akaamua kuhama mtaa.
Story nyingine ambayo Banana
ameshea na sisi amesema mama yake aliwahi kumwambia kuwa asimuumize
mwanamke yoyote wala kumpiga.. hajawahi kuchepuka wala kufumaniwa kwa
sababu yeye kama kioo cha jamii anapenda kuwa mfano wa kuigwa.
Kusikiliza stori yote bonyeza play hapa chini…
0 comments:
Post a Comment