Kwenye zile stori za City to City,Nation to Nation nimekutana na hii kutoka kwa Chege Chigunda ambaye wiki 3 zilizopita nilikutana nae South Africa na alikua ameenda kufanya kazi na mmoja wa wasanii wa kundi la Mafikizolo,leo nakusogezea nyingine kutoka kwa mkali huyo huyo anaewakilisha familia ya Tmk Wanaume Family.
Chege aliposikika kwenye Amplifaya alisema kuwa mbali na kumshirikisha moja kati ya memba wa Mafikizolo pia ana kazi nyingine ambayo amempa Kolabo mkali anaechipukia kwa sasa Nigeria anaitwa Runtown,sasa hivi Chege yuko Nairobi na ameenda kwa ajili ya kazi moja tu ya muziki.
Muziki uliompeleka Chege Nairobi si muziki wa kurekodi yeye hapana ni muziki ambao kaombwa na Nonini kufanya nae Kolabo,Chege na Nonini haitokua singo ya kwanza kusikika pamoja ipo singo pia waliyofanya pamoja inaitwa Kila mmoja ambayo alishirikishwa pia na Lady B.
Sasa hivi Chege bado yuko Nairobi kukamilisha kolabo ya Nonini inayoitwa Wanajishuku imerekodiwa studio zinazoitwa Ingoma na upande wa video imeongozwa na Director anayeitwa Willie kutoka +254 Kenya,nimepata baadhi ya picha mtu wangu.
0 comments:
Post a Comment