Mshambuliaji wa muda mrefu katika klabu ya Simba Musa Hassan Mgosi August 7 amefunguka kuhusiana na maisha ya Congo namna watu wanavyoishi, Mgosi ambae aliondoka Simba mwaka 2011 na kuelekea katika klabu ya DC Motema Pembe ya Congo Kinshasa kabla ya mwaka 2015 kurudi katika klabu yake ya zamani Simba.
Kulikuwa kuna story mtaani kuwa maisha ya Congo
watu wanakula nyani kama nyama ya ng’ombe, na upatikanaji wa nyama ya
ng’ombe ni mgumu na wa gharama, hata hivyo gharama sio sababu ya watu wa
nchi hiyo kula nyani ni kama utamaduni wa nchi hiyo, zote hizo zilikuwa
tu story lakini hazikuwa na uthibitisho.
Team ya RuAhaToWn.Com ilimtafuta Musa Mgosi
kama mmoja wa Watanzania waliowahi kuishi huko ni kweli watu wanakula
nyama ya nyami na yeye alikuwa anakula nini wakati yupo huko?
“Nikweli
unajua kila nchi inakuwa na utaratibu wake na falsafa zake kuhusu
masuala ya msosi kwangu mimi binafsi nilikuwa sipendi kula ma hotelini
kwa hiyo mimi nilikuwa naenda kwenye supermarket naweza nikanunua viazi,
mchele na maharage vitu ambavyo vya kawaida kwa chakula cha
Mtanzania”>>>Mgosi
Msikilize Mgosi zaidi hapo chini maisha aliyoyakuta Congo
0 comments:
Post a Comment