Professor Jay kapita kura za maoni Ubunge huu hapa


Stori ninayotaka kukusogezea ni hii kutoka kwa mkongwe wa Hip Hop Joseph Haule aka Professor Jay ambaye wiki zilizopita alishinda kura za maoni kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo katika Jimbo la mikumi Morogoro.
Sasa leo Agosti 7, 2015 amekutana na ripota wa TZA na kupiga naye stori kuhusiana na mchakato wa kura za maoni jinsi ulivyofanyika.
.
.
‘Namshukuru  Mungu kura za maoni zimeenda vizuri, niwapongezi tu watu wa CHADEMA kwa kutimiza demokrasia na tuliweza kupga kura na nimeweza kuibuka mshindi baada ya kupata kura 240 n Mpinzani wangu  DR. Salvatory Makweta 18, Brendan Maro 15, Mkumbata 5 lakini niseme kwamba ule ushindi sio kuonesha Jay ameshinda au anajua sana nawashukuru sana watia nia wote walikuwa wana nguvu na wote walikuwa na uwezo’- Professor Jay 
.
.
‘Baada ya kushinda kura za maoni nimepita kuwashukuru wananchi kwa kunichagua wajua wa kamati kuu zile za kata lakini pia nimewaomba watia nia wenzangu wahusike moja kwa moja kwenye hizi kampeni na kwa moyo wamekubali na ndio wataendeza kampeni zangu kwasababu naamini kupitia elimu zao kila kitu kitaenda sawa’ – Professor Jay
.
.
‘Pamoja nimechaguliwa kuendelea kuwatumikia wananchi wa Mikumi  kazi zangu za Muziki nitaendelea kuufanya kwasababu muziki ndio maisha yangu na nitakufa nikiendelea kufanya muziki ila nitakuwa sifanya kwa mashindano bali muziki wangu utakuwa wa Level juu kwa hiyo nitakuwa nafanya mara chache kwa level ya juu zaidi, mashabiki wangu watambue kuwa nipo kwaajili yao na sitawangusha’ – Professor Jay
Share on Google Plus

About Global Publishers

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment